Jumla ya watoto 28,141 wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wamepatatiwa matone ya Vitamini A katika zoezi la kampeni ya Vitamin A kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano lililofanyika tarehe 1 hadi tarehe 30 Juni mwaka huu.
Akitoa taarifa ya zoezi hilo katika Kikao cha Kamati ya Lishe cha kichofanyika leo tarehe 22/08/2023 Mratibu wa Lishe wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Bi. Hadija Kitumpa alisema zoezi hilo limehusisha vituo 33 vinavyotoa huduma ya mama na mtoto katika Manispaa ya Moshi.
Kitumpa amesema matone ya Vitamin A yanasaidia kinga ya mwili wa mtoto dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumwezesha mtoto kuona vizuri .
Aidha aliwataka wajumbe kuhamasisha kuhusu umuhimu wa unyonyeshaji kwa watoto maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo.
” Maziwa yamama kwa miezi sita ya mwanzo ni muhimu sababu maziwa ya mama yana kinga ya kutosha kwa mtoto, yanawezesha mtoto kuweza kukua vizuri kimwili na kiakili na ni chakula chenye virutubishi vyote kwa mtoto” Alisema Kitumpa