Karibu kwenye tovuti yako pendwa ya Lishe4life.com “Lishe kwa Maisha”, chanzo namba moja cha kuaminika kuhusu makala za masuala ya lishe na afya. Katika Dunia inayobadilika kila wakati, tunatoa taarifa zilizothibitishwa, za kisayansi na zinazoweza kutekelezeka ili kuboresha afya na Lishe ya jamii.
Lishe4life au “Lishe kwa maisha” ni tovuti ambayo imeundwa kwa kuzingatia dhana inayosisitiza umuhimu wa lishe bora kama mahitaji ya msingi na endelevu katika maisha yote kwa ajili ya afya na ustawi jamii. Dhana hii inaakisi imani kwamba lishe bora sio jambo la kuzingatiwa kwa muda mfupi tu bali ni suala muhimu katika maisha yetu kuanzia wakati wa mimba, kuzaliwa hadi uzee.
Lengo la tovuti ya Lishe4life.com ni kuifahamisha na kuielimisha jamii, kutoa miongozo ya lishe ili kuisaidia jamii kuelewa umuhimu wa lishe bora kupitia taarifa sahihi na miongozo sahihi ya lishe kwa Afya bora.
Kuanzishwa kwa Lishe4life.com kutawezesha maelfu ya Watanzania kupata elimu ya Lishe. Kupitia juhudi za tovuti hii na mipango mingine iliyoanzishwa timu ya Lishe4life.com Tanzania itashuhudia mabadiliko chanya katika afya ya jamii.