Karibu kwenye kikokotoo cha BMI kutoka Lishe4life.com! BMI ni kifupi cha “Body Mass Index” au “Uwiano wa Uzito na Urefu” kwa Kiswahili. Kikokotoo hiki kitakusaidia kutambua zaidi kuhusu afya yako kwa kuzingatia uzito wako na urefu wako.
Jinsi ya Kutumia Kikokotoo:
- Weka uzito wako katika kilogramu.
- Weka urefu wako katika sentimita.
- Bonyeza ‘Kokotoa’ ili kupata matokeo yako.
Matokeo ya BMI:
- Chini ya 18.5: Uzito pungufu
- 18.5 – 24.9: Uzito wa kawaida
- 25.0 – 29.9: Uzito wa ziada
- 30.0 na zaidi: Unene (obesity)
Kikokotoo cha BMI (Uwiano wa uzito na urefu)
require | require |
Uwiano wa uzito na urefu/BMI yako ni......
BMI | Tafsiri ya viwango vya BMI |
---|---|
Chini ya 18.5: | Uzito pungufu (Underweight) |
18.5 - 24.9: | Uzito unaofaa (Normal weight) |
25 - 29.9: | Uzito Uliozidi (Overweight) |
30 - 34.9: | Unene uliokithiri/Kiribatumbo (Class I Obese) |
35 - 39.9: | Unene uliokithiri/Kiribatumbo (Class II Obese) |
40 na zaidi: | Unene uliokithiri/Kiribatumbo (Class III Obese) | FOMULA ILIYOTUMIKA: | BMI=Uzito(kg)/Urefu(m)xUrefu(m) |
Faida za Kujua BMI Yako:
Kujua BMI yako kunaweza kukusaidia kuelewa:
- Hali ya mwili wako kuhusu uzito.
- Hatari zinazoweza kutokea kwa afya yako kutokana na uzito wako.
- Hatua unazohitaji kuchukua ili kuimarisha afya yako.
Kumbuka: Ingawa BMI ni zana nzuri ya kutambua hali yako ya Lishe, lakini siyo kipimo kamili. Kwasababu haitoi picha kamili ya hali ya lishe kwa watu wenye misuli mingi ya mwili. Kwa ushauri zaidi kuhusu uzito wako na afya yako, ni vizuri kuwasiliana na daktari au mtaalamu wa lishe.