Akifungua kikao hicho Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Omary Mkangama amesema kuwa suala la lishe ni jambo la Kitaifa ambalo limepewa kipaumbele kwani Mkataba shule kwani Mkataba wa lishe umeanza kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na imeshuka chini hadi kwa watendaji wa Vijiji.
Bw. Mkangama amesema kuwa kila Idara au sekta ihakikishe kwamba afua za lishe zinafuatwa na kutekelezwa kwa kuzingatia Muongozo wa lishe kwa kufanya hivyo italeta tija kwa Halmashauri na Jamii kwa ujumla.
Pia Bw. Mkangama ametoa maelekezo kuwa ratiba za vikao vyote vya lishe kwa mwaka wa fedha 2023/2024 visomeke kwenye ratiba za vikao vya Halmashauri.