Maagizo hayo yametolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Ndg. Said Kitinga akiongoza kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa robo ya nne Aprili –Juni kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya.
Akifungua Kikao hicho Ndg Kitinga amewaeleza wajumbe kuwa Lishe ni Msingi wa kila kitu na kikao hicho ni muhimu katika uboreshaji wa Lishe katika Jamii.
Akizungumza katika kiko hicho Kitinga amewataka Maafisa Watendaji wa Kata kufanyia kazi makubariano ya kikao. Pia kutumia vikao na mikutano katika Kata zao kwa kutoa Elimu ya lishe ikiwa ni pamoja na kuwaalika Maafisa Lishe katika vikao hivyo , ili kuongeza Lishe bora katika Jamii.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt Nuru Yunge amewahimiza Watendaji wa Kata zote 26 kuendelea kusimamia na kufwatilia upatikanaji wa lishe bora katika Kata zao kwa kuzingatia vigezo vya Taifa kwa kuendelea kutoa Elimu ya umuhimu wa lishe bora pamoja na madhara ya lishe duni.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia Shule zote zinatoa chakula cha mchana kwa Wanafunzi.