Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Emmanuel Mkongo ameongoza Kikao cha ndani kujadili utekelezaji wa Afua za Lishe ndani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Idara mtambuka zinazohusika za zoezi la Lishe ziliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe katika maeneo yao kwa kipindi kizima cha robo ya nne Aprili – June 2023 na kuelezea mafanikio yaliyopatika katika kipindi hicho pamoja na mapungufu yaliyojitokeza na kuonesha mikakatiti ya kukabiliana nayo kwa kipindi cha Mwaka mpya wa 2023/2024.
Aidha, Kikao kimeelekeza kuendelea kutoa Elimu na hamasa kwa wakazi wa Bunda Mji kuendelea kuchangia vyakula mashuleni ili watoto wao wapate chakula na kisha kupokea vizuri mafundisho toka kwa walimu wao.
Kikao kimeazimia pia kuendelea kutoa Elimu ya Lishe kwa wazazi wa watoto chini ya miaka mitano kuzingatia vyakula vyenye virutubisho lishe kwa watoto wao ili wakue vyema wakiwa na afya njema na kuepuka magonjwa yatokanayo na lishe duni.
Aidha kupitia Idara husika, kikao kimeelekeza kutoa elimu kwa wakazi a Bunda kupanda miti ya matunda katika maeneo na mashamba yao ili kuongeza upatikanaji wa matunda katika milo yao.