Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Chato Kwa kushirikiana na wadau (USAID) Yametolewa Leo Agost 15, Kwa vijiji 10 na kata 7 ambapo washiriki ni wauguzi pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii Ili kupambana na udumavu wa watoto uliofikia 38.6% Mkoa wa Geita.
Afsa Lishe Wilaya Bw- Renatus Kimba ametoa ufafanuzi juu ya Lishe bora Kwa jamii, na kufundisha makundi matano ya chakula kuwa ni Vyakula vya nafaka mizizi na ndizi mbichi, Vyakula vya asili ya wanyama na jamii ya mikunde, mbogamboga, mafuta na matunda. Pamoja na kuyajua pia amewafundisha na umuhimu wake.
Sambamba na hayo amewasisitiza wauguzi na watoa huduma ngazi ya jamii (wahudumu wa afya) kuyaelewa makundi hayo ya vyakula Ili kuweza kusaidia jamii kuwa na Lishe bora inayofuata mtiririko wa vyakula Ili kuepuka kula mlo unaofanana au kula mlo Mmoja usio na virutubisho.
Sanjali na hayo pia wamesisitizwa juu ya usafi wa Vyakula, vinywaji na mazingira Ili kuweza kujikinga na vyanzo vya magonjwa vinavyoweza kupelekea afya kudorola na kurudisha nyuma ukuaji wa mtoto.