Akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Z. Stephen kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni amewataka wajumbe wa kikao hicho kufahamu kuwa lishe ndiyo kila kitu na kwamba kikao hicho ni muhimu sana katika uboreshaji wa lishe katika Jamii ili kuondokana na udumavu.
Pia amepongeza utekelezaji wa afua za lishe na kuwataka Watendaji wa Kata kufanaya vikao na kutoa elimu kuhusu lishe kwenye Kata zao na kuweka maazimio kuhusu utekelezaji wa afua za lishe na ili kufikia malengo
Aidha Mkurugenzi Mtendaji ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Kata zote kuwa kuhakikisha wanasimamia shule zote zinatoa chakula na wanafunzi wote wanapata chakula cha Mchana wawapo shuleni.
Maafisa Watendaji wa Kata zote 21 za Halmashauri wamekubaliana kuendelea kusimamia na kufuatilia upatikanaji Lishe katika kata zao kwa kuzingatia vigezo vya Kitaifa kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa lishe bora pamoja na madhara ya lishe duni.